Bwana humjaribu mwenye haki; bali nafsi yake humchukia asiye haki, na mwenye kupenda udhalimu… —ZABURI 11:5
Wakati mwingine walimu huacha wanafunzi kujibu maswali ya mtihani kwa kurejelea vitabu vilivyo na majibu. Huruhusiwa kuwa na vitabu vya kurejelea wanapojibu maswali. Tutafanya mitihani sisi wote. Hakuna atakayekosa kuifanya—kila mtu hujaribiwa kwa wakati tofauti katika maisha. Lakini yote mitihani inayofanywa kwa kurejelea vitabu; majibu hupatikana katika Kitabu. Hata kama tunapitia hali gani, Mungu ametoa majibu katika Neno lake.
Kumkaribia Mungu kupitia kwa neno lake tunapopitia wakati mgumu hutupatia nguvu na majibu tunayohitaji. Wakati mwingine huruhusu tupitie mahali pagumu kwa sababu anatufanyisha mtihani, kutupanua na kutuimarisha. Wakati kama huo, shetani hutushambulia katika mawazo, akituambia uongo kama, “Mungu hakupendi, na kama alikuwa akusaidie, angelishafanya hivyo tayari. Unaweza pia kukata tamaa kumtumainia Mungu na kuanzisha mpango wako wa kukwepa.” Huu ni wakati wa kushikilia, sio kukata tamaa!
Maisha wakati wote huwa si rahisi. Kutakuwa na baadhi ya siku na misimu ambapo tutakabiliwa na changamoto. Lakini ukichagua kumwegemea Bwana katika nyakati hizo, utagundua kuwa unaweza bado kuwa na furaha hata katika siku za majaribu. Nguvu za kiungu, hekima na maarifa, ukomavu wa kiroho na mienendo mizuri inakuzwa ndani yetu tunapopitia majaribu.
Ili kukua ndani ya Mungu na kufanya alichokuita kufanya, chagua kuwa mwaminifu. Mwenendo wake utatokea katika maisha yako polepole.