Mkumbushe Mungu Neno Lake

Nimeweka walinzi juu ya kuta zako, Ee Yerusalemu; hawatanyamaza mchana wala usiku; ninyi wenye kumkumbusha Bwana, msiwe na kimya (ISAYA 62:6)

Andiko la leo linatuagiza kumkumbusha Mungu kuhusu ahadi alizofanyia na mojawapo ya njia nzuri za kufanya hivyo ni kuomba kwa kumwambia  Neno lake.

Neno la Mungu ni la thamani sana kwake na linafaa kuwa hivyo kwetu pia. Isitoshe huzungumza nasi kwa uwazi kupitia kwa Neno lake na njia ya kuaminika ya kusikia sauti yake. Kwa kweli, tafsiri ya Biblia ya Amplified inasema ifuatavyo katika Zaburi 138:2: “Nitasujudu nikilikabili hekalu lako takatifu, nitalishukuru jina lako, kwa ajili ya fadhili zako na uaminifu wako kwa maana umeikuza ahadi yako, kuliko jina lako lote!” Hili andiko huonyesha kwamba Mungu hulikuza Neno lake hata juu ya jina lake. Iwapo analiheshimu neno lake kwa namna hiyo, tunahitaji kulipa Neno kipaumbele cha kulijua, kusoma Neno, kupenda Neno, kupanda Neno kabisa katika mioyo yetu, kuinua Neno zaidi kuliko kitu kingine chochote na kujumlisha Neno katika maombi yetu.

Tunapoheshimu Neno na kujikabidhi kwalo vile nilivyoeleza, “mnakaa” ndani yake (soma Yohana 15:7). Kukaa ndani ya Neno na kuruhusu Neno kukaa ndani yetu ina uhusiano na uhakika katika maombi na kujibiwa kwa maombi yetu. Tunapoomba Neno la Mungu, itakuwa si rahisi kuomba vitu ambavyo si mapenzi ya Mungu kwa ajili yetu.

Yesu Kristo ndiye Neno linaloishi (soma Yohana 1:1-4), na tunapoendelea kukaa katika Neno, tunakaa ndani yake- na hilo linaleta nguvu za ajabu katika maombi yetu.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Neno la Mungu hugeuza kwa kufanya upya nia yako na kukufundisha kufikiri vile Mungu anavyofikiria.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon