Mpango Mzuri wa Mungu

Mpango Mzuri wa Mungu

Macho yako yaliniona kabla sijakamilika; chuoni mwako ziliandikwa zote pia, siku zilizoamriwa kabla hazijawa bado. — ZABURI 139:16

Mungu alikuwa na mpango mzuri aliopangia kila mmoja wetu kabla tutokee katika sayari hii. Na mpango wake wa kipekee kwa kila mmoja wetu sio wa ushinde na kila aina ya taabu.

Katika Yohana 10:10, Yesu anasema, “Mwizi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; Mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.” Shetani huja kuharibu kitu kizuri ambacho Mungu anawaza kwa ajili yetu na tunahitaji kumpinga kwa uthabiti.

Huenda mpango mzuri wa Mungu ulikatizwa katika maisha yako, lakini hujachelewa! Mungu anakufikia sasa na kutaka kukurejeshea kitu chochote ambacho adui ameiba, na kukupa baraka maradufu kwa sababu ya mashaka uliyopitia (Zekaria 9:12). Muombe afanye hivyo, kisha umtazame akifanya kazi maishani mwako.


Mungu atakufanyia usiyoweza kujifanyia.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon