Msamaha: njia ya amani halisi na furaha

Msamaha: njia ya amani halisi na furaha

Bali wapendeni adui zenu, tendeni mema, na kukopesha msitumaini kupata malipo, na thawabu yenu itakuwa nyingi; nanyi mtakuwa wana wa Aliye juu, kwa kuwa yeye ni mwema kwa wasiomshukuru, na waovu. Luka 6:35

 Miaka michache iliyopita mtu fulani aliniambia kuhusu mtu ambaye alikuwa akifanya biashara na huduma yetu. Rafiki yangu alikuja kwenye mkahawa huo huo, akaketi kwenye kibanda kilichofuata, na aliposikia mazungumzo yao, ambayo yalitokea tu kuhusu mimi-na hawakusema mambo mema kamwe.

Mwanzoni nilikasirika na nilitaka kumwambia kuwa hatawahi kupata tena biashara yetu. Lakini usiku huo, Roho Mtakatifu akaniambia, “Huwezi kufanya mambo hayo kamwe.” Akasema, “Hapana, utaenda kufanya yale unayofundisha. Wewe utaenda kumpea zawadi, na kumwambia jinsi unavyopenda sana huduma ambazo amekupa miaka yote hii. ”

Haikuwa rahisi, lakini Mungu alinipa neema ya kutii mwelekeo Wake na kuwa baraka kwa mtu huyu.

Kile nakumbuka zaidi juu ya hali hii ni kwamba mara tu nilipoanza kuchukua hatua ya kufanya jambo jema kwake, nilikuwa na furaha ya kufanya hivyo.

Wakati tunaweza kuangalia watu ambao wametuumiza kwa huruma, kuna sherehe inayoendelea ndani yetu kwa sababu ya jinsi furaha ya Mungu inaijaza nafsi yetu.

Kwa hiyo ni nani ambaye unaweza kumsamehe na kufanya kitu kizuri kwake leo? Jifunze msamaha na ufuate njia inayoongoza kwa amani halisi na furaha!

 OMBI LA KUANZA SIKU

Mungu, ninahitaji neema yako kutii Neno lako na kufanya mema kwa wale ambao wameniumiza. Najua kwamba kama ninasamehe na kuwabariki, Utanipa amani na furaha katika nafsi yangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon