Mungu Ataridhisha Matamanio Yako

Kama ayala aioneavyo shauku mito ya maji… vivyo hivyo nafsi yangu inakuonea shauku, Ee Mungu. Nafsi imemwonea kiu Mungu, Mungu aliye hai… (ZABURI 42:1-2)

Nilienda kanisani kwa kipindi cha miaka mingi bila kujua kwamba Mungu alikuwa anataka kuzungumza nami, hata ingawa nilimpenda kwa dhati. Nilitii kila kaida za kidini na likizo na kuhudhuria kanisa kila Jumapili. Nilifanya kila kitu nilichojua kufanya wakati huo, lakini havikutosha kuridhisha matamanio yangu ya Mungu.

Nilitumia kila muda wangu kuwa kanisani au katika mafunzo ya Biblia, lakini hayo hayakutuliza kiu yangu ya kutaka uhusiano wa ndani na Bwana. Nilihitaji kuzungumza naye kuhusu mambo yangu yaliyopita na mimi nimsikize akizungumza nami kuhusu mstakabali wangu. Lakini aliyenifunza kwamba Mungu alitaka kuzungumza nami moja kwa moja. Hakuna aliyenipa suluhu ya matamanio yangu ya kiroho.

Kupitia kwa kusoma Biblia, nilijifunza kwamba, Mungu anataka kuzungumza nasi na kuridhisha matamanio yetu ya uwepo wake na mwingiliano wake katika maisha yetu. Ana mipango juu ya maisha yetu- mipango ambayo itatuongoza katika amani na ridhaa, na anataka tupate maarifa na ufahamu wake na mapenzi yake kupitia kwa uelekezi wa kiungu.

Mungu anahusika katika kila kitu kinachokuhusu na mpango wake ni kuhusika kwa undani katika kila kipengele cha maisha yako. Kujua na kuamini ukweli huu umefanya kutembea kwangu naye kuwe tukio lisilo la kawaida badala ya wajibu wa kidini.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Tumia sehemu ya muda wako mtulivu leo kuwa mtulivu! Kuwa mtulivu na utafute kusikia kile ambacho Mungu anataka kukuarifu.   

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon