Mungu Hutuongoza Kutoka Hatua Moja Hadi Nyingine

Mungu Hutuongoza Kutoka Hatua Moja Hadi Nyingine

Hatua za mtu zaimarishwa na Bwana, naye aipenda njia yake. Ajapojikwaa hataanguka chini, Bwana humshika mkono na kumtegemeza. ZABURI 37:23–24

Tunapopitia maisha haya, kila mmoja wetu anaitwa kuwa na safari binafsi na Mungu. Shukuru kuwa, Mungu hutupatia mwelekeo tunaohitaji, akituonyesha njia ya kupitia na, kwa usaidizi wake tunamfuata.

Safari na Mungu hufanyika kupitia kwa hatua moja ya imani kwa wakati. Baadhi ya watu hutaka mpango mzima wa maisha yao kabla ya kufanya uamuzi mmoja, lakini Mungu mara nyingi huwa hafanyi kazi hivyo; anatuongoza siku baada ya nyingine. Kwa kuwa hatujui kila kitu kilicho mbele yetu, tunahitaji kuishi kwa imani, na hivyo ndivyo Mungu anataka.

Kwa imani, tunachukua kila hatua ambayo Mungu ametuonyesha, halafu anatupatia inayofuatia. Wakati mwingine huenda tukaanguka chini, lakini tunaweza kushukuru kwamba Mungu hutusaidia kuinuka. Tunaendelea kwa nguvu zake na neema zake, tukijua kwamba kila wakati tunahitaji kufanya uamuzi, Mungu atatuongoza kwa sababu tuna uhusiano wa kibinafsi naye.


Sala ya Shukrani

Ninakushukuru leo, Baba, kwamba unaniongoza hatua moja kwa wakati mmoja. Ninaamini mwelekeo wako juu ya maisha yangu. Ninakushukuru kuwa mpango wako kwangu ni mwema na hutawahi kunipoteza.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon