Mwanzo, Katikati, na Mwisho

Heri mwisho wa neno kuliko mwanzo wake , na mvumilivu rohoni kuliko mwenye roho ya kiburi. —MHUBIRI 7:8

Kitu muhimu kabisa sio tu vile tunavyoanza kitu. Mwanzo ni muhimu, lakini katikati pia, na mwisho pia. Kwa kweli, kuona kitu kimekamilika ni muhimu zaidi kuliko tu kukianzisha, haswa kikiwa kitu ambacho Mungu ametuita kufanya.

Watu wengine huanza kwa fujo, lakini huwa hawamalizi. Wengine ni waanzilishi wa polepole, lakini humaliza wakiwa na nguvu. Haijalishi tunavyoanza, Mungu anataka tuwe waaminifu katika kila hatua njiani—mwanzo, katikati na mwisho. Matamanio ya Mungu ni wewe kumaliza vizuri.

Mungu ana mpango mzuri kwa kila mmoja wetu. Lakini ni uwezekano, sio “uchanya.” Haitafanyika vizuri tusiposhirikiana na Mungu. Tuna sehemu yetu ya kufanya ili kuhakikisha kwamba mpango huo unafanikiwa. Mungu hawezi kufanya kitu chochote katika maisha yetu bila ushirika wetu.

Ninakutia changamoto kushirikiana na Mungu kila siku ya maisha yako ili ukuze uwezo wako na kutazama mpango wake ukija kutimia. Unaweza kujfunza kitu kipya kila siku. Unaweza kupiga hatua kuliko ya siku iliyotangulia kila siku. Unaweza kukua kila siku. Hivi ndivyo unavyogeuza mwanzo mkuu hadi hata kuwa mwisho bora zaidi.


Shirikiana na Mungu ili kukuza vipawa, talanta na uwezo wako hadi kwenye ukamilifu. Kuwa unachoweza kuwa kwa utukufu wa Mungu!

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon