Neema ni Nini?

Neema ni Nini?

. . . Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa kwayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho wa neema. —WAEBRANIA 10:29

Neema ni nguvu ya Roho Mtakatifu iliyopo kwa ajili yako ili ikuwezeshe kufanya kwa urahisi mambo usioweza kufanya kwa kung’ang’ana kwa nguvu zako. Neema ni nguvu za Mungu zinazokuja katika maisha yetu, kwa uhuru zikituwezesha kufanya tunayohitaji kufanya. Neema ya Mungu huwepo kila wakati, lakini tunahitaji kuipokea kwa neema na kukataa kufanya mambo kwa nguvu zetu peke yetu bila Mungu.

Roho Mtakatifu hutupatia neema kutoka kwa Mungu Baba. Neema kwa kweli ni nguvu za Roho Mtakatifu zinazotiririka kutoka kwa kiti cha enzi cha Mungu hadi kwa watu ili kuwaokoa na kuwawezesha kuishi maisha matakatifu na kutimiza mapenzi ya Mungu.

Tunaweza kufurahia na kuwa na wingi wa amani, furaha, na kuridhika kila siku kwa sababu ya neema ya Mungu katika maisha yetu. Ni neema yake inayoturuhusu kuishi katika ushirika wa karibu naye. Tukiwa na neema ya Mungu, maisha yanaweza kufurahiwa kwa utulivu unaozaa kupumzika na kuridhika.


Tumeokolewa kwa neema kupitia kwa imani, na tunafaa kujifunza kuishi vivyo hivyo!

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon