Neno la Maarifa

… na mwingine neno la maarifa… (1 WAKORINTHO 12:8)

Neno la maarifa hutumika kwa njia moja na neno la hekima. Kuna fasiri nyingi tofauti za neno la maarifa, lakini wengi wanakubali kwamba hutumikishwa wakati ambao Mungu anamfunulia mtu kitu kuhusu atakachofanya katika hali fulani, iwapo mtu anayepokea maarifa hayo asingekuwa na njia ya kawaida ya kujua.

Wakati mwingine Mungu anapozungumza nasi na kutupatia neno la maarifa kuhusu watu wengine, tunajua kuna kitu kibaya kuwahusu au tunajua wanahitaji kufanya kitu fulani katika hali maalum. Hatufai kujaribu kumlazimisha mtu kukubali aina hii ya maarifa ya kimiujiza. Badala yake, tunafaa kuyawasilisha kwa unyenyekevu na kuacha Mungu amshawishi. Wakati mwingine kile Mungu hutaka tufanye ni kuombea mtu huyo.

Huku neno la maarifa likipeanwa mara nyingi kama kifaa cha huduma cha kusaidia wengine, ni la thamani sana pia katika maisha yetu binafsi. Kwa mfano, hii karama hutumikishwa sana ninapopoteza kitu au kusahau nilipokiweka. Huwa sikumbuki nilipoweka kitu, halafu ghafla Roho Mtakatifu ananipa picha akilini, wazo au neno kuhusu mahali kilipo. Huu ni mfano tendaji kuhusu alivyonipa maarifa ambayo kwa kawaida sikuwa nayo na njia ambayo neno la maarifa hutumikishwa katika maisha yako pia.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Elimu ni bora, lakini maarifa ya Mungu ni bora zaidi, kwa hivyo hakikisha unamtegemea.  

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon