Nguvu ya Kukiri

Nguvu ya Kukiri

Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; na wao waupendao watakula matunda yake. —MITHALI 18:21

Tukitaka kuona maombi yetu yakijibiwa, ni muhimu kujifunza kuomba kisha tukiri maneno mazuri yaliyojaa imani kuhusu hali zetu. Kukiri maneno mabaya na imani haviendi tu pamoja.

Hebu tuseme mama anaombea mtoto wake wa kiume ambaye ana matatizo shuleni. Kwa hivyo anaomba maombi ya imani na kumwamini Mungu kwa mpenyo. Kisha anaenda kwa chakula cha mchana na majirani wawili na kutumia lisaa linalofuatia akisema, “Nimechoka kuhusu haya matatizo yote niliyo nayo na mwanangu. Mambo hayatabadilika. Kwa nini mimi? Kukiri kubaya kwa aina hii hufanya kazi kinyume na imani yako.

Baada ya kuomba, fanya uamuzi wa kufanya mazungumzo yako yakubaliane na maombi yako. Kiri Neno la Mungu! Kiri imani yako! Majirani wakiuliza vile mwanao anaendelea, sema, “Unajua nini? Katika mwili, vita havijabadilika sana, lakini ninamwombea, na nina hakikisho katika moyo wangu kuwa Mungu yuko naye, na anafanya kazi kubwa katika maisha yake.”

Imani yako, mawazo yako na maneno yako vyote vikikubaliana, ni muda tu na utaona mabadiliko mazuri.


Omba kisha uache kila unachosema kikubaliane na kile umeomba na kwa kweli utaona matokeo ya ajabu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon