Nia ya Kristo

Nia ya Kristo

. . . Maana ni nani aliyeifahamu nia ya Bwana, amwelimishe? Lakini sisi tunayo nia ya Kristo. —1 WAKORINTHO 2:16

Mimi na wewe tumepewa nia ya Kristo—hii ni ahadi inayotoka katika Neno la Mungu moja kwa moja. Ili kuanza kuelewa inachomaanisha, fikiria vile nia ya Yesu ilivyokuwa alipokuwa akiishi ulimwenguni. Alikuwa na hakika ya yule aliyekuwa. Hakuacha maneno hasi ya wengine yamzuie. Alijua kitimilifu kwamba alipendwa na Mungu. Na alidhamiria kutimiza mpango wa Mungu kwa ajili ya maisha yake.

Sasa chukua muda mfupi kufikiria mawazo ambayo hushughulisha nia yako. Iwapo unaondolewa kwenye shughuli zako na maoni ya wengine, iwapo unakasirika haraka, au iwapo nia yako imejaa shaka na kutokuamini, bado hujaanza kufurahia matamanio yote ya Mungu juu ya maisha yako. Lakini vitu vinaweza kubadilika. Mungu anaweza kugeuza nia yako na kukuleta mahali pa ushindi!

Ugeuzwaji wa nia ni mchakato ambao unahitaji muda, na mchakato ambao adui hupinga vikali. Ni muhimu kwetu sisi kuchagua kuwa na mawazo mazuri kimaksudi. Tunapohisi vita vya nia yetu ni vigumu, tunaweza kuamua kwamba, kwa usaidizi wa Mungu, tutachagua kimaksudi mawazo yanayoleta uzima.

Ugeuzwaji wa nia hufanyika polepole, kwa hivyo usikate tamaa iwapo unaonekana kupiga hatua polepole. Chukua msimamo na useme, “Sitawahi kukata tamaa! Mungu yuko upande wangu. Ananipenda, na ananisaidia!”


Mawazo yetu huathiri mtu wa ndani, afya yetu, furaha yetu na nia zetu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon