Lakini mimi nawaambia, wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi (MATHAYO 5:44)
Mojawapo ya maombi ya nguvu sana unayoweza kuomba ni maombi kwa maadui zako. Ukitaka kuona mtu aliye na nguvu katika maombi, tafuta mtu akayeomba kwa niaba ya adui. Ninaamini kwamba Mungu hutubariki kwa njia kuu tunapoombea waliotukosea au kutusaliti.
Je, unamkumbuka Ayubu? Aliwaombea rafiki zake baada ya wao kumumiza moyo na kumsikitisha. Lakini punde tu baada ya kuwaombea, Mungu alileta urejesho katika maisha yake. Kwa kweli, Mungu Mungu alimregeshea vitu maradufu ya vile ambavyo alikuwa amepoteza (soma Ayubu 42:10)! Kuombea mtu aliyetukosea ni jambo la nguvu kwa sababu, tunapofanya hivyo tunatembea katika upendo kwa mtu huyo na tunatii Neno la Mungu.
Tunaweza kusikia sauti ya Mungu katika andiko la leo. Yesu anatuambia kufanya nini katika andiko hili? Anatuagiza kuombea adui zetu. Unapofikiria kuhusu watu waliokutumia, kukudhulumu, kukukasirisha, na kuzungumza maovu kukuhusu, wabariki; usiwalaani. Waombee. Mungu anajua kwamba kubariki adui zako si rahisi na huenda usihisi kufanya hivyo. Lakini hufanyi hivyo kwa kuwa unahisi kufanya hivyo; unafanya hivyo kama ambaye unamfanyia Mungu. Kuchagua kuomba na kubariki badala ya kulaani kuna nguvu katika ulimwengu wa kiroho, na Mungu atafanya mambo makubwa katika maisha yako kutokana na hilo.
NENO LA MUNGU KWAKO LEO:
Usiruhusu watu walio na roho ya uchoyo wakushukishe hadi katika kiwango chao kwa kukujaribu kutenda wanavyotenda.