Orodha ya Shukrani ya Mtume Paulo

Orodha ya Shukrani ya Mtume Paulo

Mungu ashukuriwe kwa sababu ya kipawa chake, tusichoweza kukisifu kama ipasavyo. 2 WAKORINTHO 9:15

Kama Yesu, Paulo alimshukuru Mungu kwa vitu vingi. Alimshukuru kwamba watu walimpokea kama mtumishi. Alimshukuru Mungu kwa washirika wake. Alimshukuru kwa makanisa aliyoanzisha. Akamshukuru kwa watu wa makanisani.

Katika 2 Wakorintho 2:14, moyo wa Paulo wenye shukrani unadhihirika anaposema : “Ila Mungu ashukuriwe, anayetushangiliza daima katika Kristo, na kuidhihirisha harufu ya kumjua yeye kila mahali kwa kazi yetu.”

Paulo alijua kwamba huwa tunapokea kila kitu kizuri ambacho Mungu amechagua kutupatia kwa neema tu. Tunaweza kufuata mfano wa Paulo na kuyaweka wakfu maisha yetu kumshukuru Mungu kwamba ametufanya kumbukumbu za ushindi wa Yesu.


Sala ya Shukrani

Ninakushukuru, Baba, kwa ushindi wa Yesu ambao huufanya wokovu wangu na maisha yangu ndani yako kuwezekana. Kama Paulo, ninataka kuishi kila siku nikiwa mwenye shukrani kwa uwezo wako na kazi yako ya ajabu katika maisha yangu. Nisaidie nisisahau kwamba neema yako humininwa ndani yangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon