Pokea Msamaha Wako

Pokea Msamaha Wako

Mimi, naam, ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi zako. —Isaya 43:25

Haijalishi shida yako ilivyo au vile unavyohisi vibaya kujihusu kutokana na hilo, tia ukweli huu katika moyo wako: Mungu anakupenda. Yesu Kristo alitwaa maisha yake ili usamehewe, na amekupa maisha mapya. Mungu amekupa familia mpya na marafiki wapya wa kukupenda, kukukubali, kukutambua na kukusaidia. Utafaulu kwa sababu ya yule anayeishi ndani yako na kukujali.

Tubu dhambi yoyote ile inayosimama kati yako nay eye na upokee msamaha. Haijalishi ulilofanya, sema, “Bwana, nilifanya, na ni jambo la ajabu mimi kutambua kwamba unanipenda pasi masharti, na kwamba unanisamehe. Umeweka dhambi zangu mbali nami kama mashariki ilivyo mbali na magharibi, na huzikumbuki tena!” (Zaburi 103:12).

Mara tu ya baada ya kutubu dhambi zako na kupokea msamaha wa Mungu, ukiendelea kuzileta mbele zake kila wakati unapoenda kwake katika maombi, unamkumbusha kitu ambacho hajasamehe tu bali kwa kweli amesahau.


Kuanzia sasa, acha kujiadhibu kwa sababu ya kitu ambacho hakipo.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon