Ridhaa ya Kweli

Naye akajibu akasema, imeandikwa mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila Neno litokalo katika kinywa cha Mungu. —MATHAYO 4:4

Sidhani kuna kitu kingine bora kuliko kuridhika. Kuamka asubuhi na kufikiria, Maisha ni mazuri: sifu Mungu, nimeridhika, na kwenda kitandani usiku kama bado umeridhika kusema kweli ni maisha yenye wingi wa baraka. Kwa upande ule mwingine, sidhani kama kitu kibaya kama kuishi katika hali ya chini ya kutokuridhika kila wakati.

Hii hapa ratili ya kupima ukweli wa kiroho: Haijalishi unachomiliki, unakoenda, au unachofanya, hakuna kinachoweza kukupatia ridhaa kando na uwepo wa kibinafsi, wa karibu na ndani na Mungu. Fedha, safari, likizo, mavazi, mambo mapya, samani mpya, nyumba mpya, kuolewa na kupata watoto, vyote ni vitu ambavyo vinaweza kutupatia furaha kiasi. Lakini hatuwezi kuwa na ridhaa ya kudumu wakati wote iwapo tutatafuta vitu vya kumiliki au kufanya ili kuziba shimo lililo ndani yetu.

Kuna waaminio wengi wasio na furaha ambao wanaishi maisha yasiyokamilika kwa sababu wanatafuta vitu visivyo! Usije ukakosa uhusiano wa kibinafsi, wa karibu na ndani na Mungu kwa sababu unatafuta kipawa badala ya Mpaji.


Vitu vya ulimwengu haviwezi kuleta ridhaa ya kweli. Mtazame Mungu kwanza na ataridhisha matamanio ya moyo wako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon