Roho Mtakatifu anatupa ushindi juu ya hisia zetu

Roho Mtakatifu anatupa ushindi juu ya hisia zetu

Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; Yohana 14:16

Adui yetu ya namba moja ni hisia. Sisi huongozwa na jinsi tunavyohisi, lakini ni lazima tuelewe kwamba hisia ni za muda na hubadilika siku baada ya nyingine. Tunapaswa kuwa makini  kutofuata kila mawazo ambayo yanakuja katika akili zetu kwa sababu mawazo yetu na hisia hazina ukweli. Kwa mfano, watu wengi wana huzuni kwa sababu hawawezi kukabiliana na ukweli, lakini Roho Mtakatifu alikuja kutufunulia ukweli. Tunapaswa kukabiliana na ukweli na kuchukua jukumu kwa vitendo vyetu, badala ya kutoa vijisababu na kulaumu mtu mwingine kwa matatizo yetu. Tunapofanya hivyo na kumwomba Mungu atusaidie, roho ya huzuni inatuacha na tunasikia kuwa wepesi na huru.

Unaweza kupata ushindi juu ya hisia zako kwa kukubali Roho Mtakatifu na kutii hekima anayofunua. Yesu alimtuma kwetu kuwa Msaidizi wetu, Mshauri, Kutuimarisha, na Kusimama ili abaki nasi milele. Tushukuru Mungu hatupaswi kuvunjwa moyo, kukata tamaa, au kufadhaika moyoni. Roho Mtakatifu anatupa ushindi juu ya hisia zetu!

OMBI LA KUANZA SIKU

Roho Mtakatifu, siwezi kudhibiti hisia zangu na tabia yangu mwenyewe. Asante kwa kunisaidia kwa kunipa uwezo wako wa kunisababishia ushindi.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon