Roho Mtakatifu Hujali Mahusiano

Wala msihuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi (WAEFESO 4:30)

Andiko la leo, kwa muktadha wa maandiko yanayolizunguka, linatufundisha  kwamba jinsi tunavyoshughulikia mahusiano ni muhimu kwa Mungu. Kuyashughulikia vibaya ni njia mojawapo tunayomhuzunisha Roho Mtakatifu.

Mara nyingi huwa tuna tabia ya kuwatesa walio karibu nasi, hususan tunapokuwa hatuhisi vizuri; hatukupata usingizi wa kutosha; tukiwa tumekuwa na siku yenye rabsha, tukiwa tumepokea habari mbaya, au kusikitishwa na mtu. Lakini Mungu anataka tuwatendee wengine mema kila wakati sio tu wakati ambao tunahisi kufanya hivyo.

Nilikuwa ninajiuliza kwa nini nilikuwa nikiwatendea wanangu na mume wangu vibaya, lakini sio watu wengine. Roho Mtakatifu akanionyesha kwamba nilidhibiti hisia zangu hasi nikiwa karibu na watu niliotaka kufurahisha. Lakini nilipokuwa na familia yangu, ambao tayari nilikuwa na uhusiano nao, nilikuwa na uhuru ambao ulionyesha wazi kasoro za tabia zangu na kutokukomaa kwa kiroho. Nikajishawishi kwamba kwa kweli nisingejisaidia, kwamba ninaponung’unika au kuwa mgumu, nisingejirudi. Nilikata tamaa nikaonekana kama ambaye nitalipuka.

Nilipofadhaika kwa sababu ya hali ngumu za kifedha, kitu kazini, au hata jambo lolote tu dogo kwa nyumba, nilimalizia hasira zangu kwa familia yangu. Wakati mwingi nilikasirika na kuwatendea vibaya kwa sababu ya kitu ndani yangu ambacho sikuwa nimekabiliana nacho, sio kwa sababu ya kile kilichokuwa kimefanyika. Mungu alinisaidia kukabiliana na ukweli na ninashukuru kwamba nimewekwa huru.

Mahusiano ni mojawapo ya rasilmali yetu kuu, na Mungu anataka tuyathamini. Roho Mtakatifu atatusaidia kushughulikia mafadhaiko yetu inavyofaa tukimkaribia kwa mioyo iliyo wazi, tayari kukubiliana na ukweli wowote anaotuonyesha.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Usiruhusu watu wengine kuteseka kwa sababu ya mafadhaiko yako ya ndani.   

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon