Roho Mtakatifu Hunena na Roho Zetu

Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, kwa sababu hawaniamini mimi, kwa habari ya haki, kwa sababu mimi naenda zangu kwa Baba, wala hamnioni tena, kwa habari ya hukumu, kwa sababu yule mkuu wa ulimwengu huu amekwisha kuhukumiwa (YOHANA 16:8)

Roho Mtakatifu huzungumza na roho zetu ili kututhibitishia dhambi na kutushawishi kuhusu haki. Uthibitisho wake unakusudiwa kutushawishi kutubu, kumaanisha kugeuka na kwenda upande ulio sawa kuliko kwenda upande usio sawa ambao huenda tayari tunaelekea.

Uthibitisho ni tofauti kabisa na hukumu. Ilinichukua muda mrefu kujifunza hivyo, na kwa sababu hiyo, kimakosa nikawa ninahukumika kila wakati Roho Mtakatifu akinithibitishia kitu katika maisha yangu ambacho hakikubaliana na mapenzi ya Mungu. Uthibitisho unakusudiwa kutuondoa kutoka kwa kitu, kutusaidia kwenda juu zaidi katika mapenzi na mpango wa Mungu juu ya maisha yetu. Hukumu kwa upande ule mwingine, hutufinyilia na kutuweka chini ya mizigo ya hukumu.

Kuhisi aibu au hukumu yenye afya tunapothibitishiwa dhambi mwanzoni ni kawaida. Lakini, kuendelea kuhisi kuhukumika baada ya kutubu dhambi hiyo si vizuri, wala si mapenzi ya Mungu. Katika kisa cha mwanamke aliyepatikana katika uzinzi (soma Yohana 8:3-11), Yesu anathibitisha kwamba hukumu huelekeza tu katika mauti, lakini uthibitisho hutuleta kwa maisha mapya yaliyo huru kutokana na dhambi.

Kwa vile Mungu hatuhukumu, tunaweza kuomba kwa ujasiri: “Bwana, nionyeshe dhambi yangu. Ifanye dhamiri yangu kuwa yenye upole kwa sauti yako. Nipe nguvu za kuwa huru kutokana na dhambi. Amina.” Kuishi hivi kutazidisha uhisivu wetu kwa sauti ya Mungu katika maisha yetu.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Shetani huhukumu; Roho Mtakatifu huthibitsha.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon