Sasa Hakuna Hukumu Ya Adhabu

Sasa Hakuna Hukumu ya Adhabu

Sasa basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu, wao wanaongozwa sio na mwili bali na Roho. —Warumi 8:1

Mojawapo ya matatizo makubwa ya Wakristo wengi ni kutokea tokea kwa kuhisi kuhukumika na kuadhibiwa kwa dhambi za kale ambazo tayari wamepokea msamaha kwazo. Furaha kuu ya shetani ni kutufanya kuhisi vibaya kujihusu, na njia moja ya kufanya hilo ni kutufanya tuhisi kuhumika. Hata kama ni hukumu ya uongo, huwa tunaathiriwa sana nayo.

Biblia inafundisha kwamba kupitia kwa damu ya Yesu, tuna msamaha mkamilifu na uhuru kamili kutokana na adhabu. Hatuna lazima ya kuongeza hukumu yetu kwa dhabihu yake msalabani. Yeye anatosha kupita kiasi.

Shetani akijaribu kuleta dhambi hiyo katika mawazo yako tena kwa njia ya hukumu na adhabu, mtangazie kwamba: “Nilisamehewa dhambi hiyo! Imeshughulikiwa; kwa hivyo, siishughulikii tena.” Utapata kwamba, kuzungumza kwa sauti mara nyingi kutakusaidia sana kwa sababu kwa kufanya hivyo, unatangaza msimamo wako juu ya Neno la Mungu. Mtangazie shetani kwamba Kristo amekuweka huru.


Usikae tu hapo na kusikiliza shutuma na uongo wa shetani. Jifunze kumjibu ukweli.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon