Sherehekea Mabadiliko

Sherehekea Mabadiliko

Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu —yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu. WARUMI 12:2 BIBLIA

Kama wana wa Mungu, tunaweza kushukuru kwa mabadiliko ambayo Mungu hufanya katika maisha yetu. Katika safari yetu hapa ulimwenguni, Roho wa Mungu atakuwa akifanya kazi nasi na ndani yetu, akitusaidia kubadilika kwa wema. Ili kupiga hatua, tunahitaji kujifungua kwa kazi ya Bwana na kuwa watiifu kwa uongozi wake.

Mungu anataka tuone ukweli (uhalisi) ili tuweze kukubaliana naye kuhusu mabadiliko yoyote ambayo yanahitajika, lakini hatuhitaji kujiadhibu tunapoona dosari au kuhisi kuhumika na kushtumiwa. Tunaweza kujisalimisha kwa Mungu na kujifunza kusherehekea mabadiliko yanayofanyika katika maisha yetu. Mabadiliko na ukuaji ni utaratibu wenye afya ambao Mungu ataendeleza mradi tu tuko duniani katika miili yetu ya kibinadamu. Mabadiliko ni kitu cha kushukuru kwacho!


Sala ya Shukrani

Ninakushukuru, Mungu, kwamba sina haja ya kuogopa mabadiliko, lakini kwamba ninaweza kufurahia ndani yake. Nisaidie kujifungua kwa uongozi wako. Ninashukuru kwa kazi yako maishani mwangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon