Shukuru Mungu kwa Fadhili Zake

Shukuru Mungu kwa Fadhili Zake

Nami nimezitumainia fadhili zako; moyo wangu na uufurahie wokovu wako. ZABURI 13:5

Bwana amejaa huruma na neema, haoni hasira upesi, ni mwingi wa fadhili (tazama Zaburi 103:8). Ni vigumu kustahili fadhili, na ndiyo kwa sababu ni kuharibu wakati kujaribu kulipia makosa yetu kwa matendo mema au hukumu. Hatustahili fadhila, lakini Mungu huitoa kwetu bure. Hiki kipaji cha bure ni kitu kinachofaa kutufanya tushukuru!

Fadhila hupuuza “kanuni.” Huenda ulilelewa katika nyumba ambayo ilikuwa na kanuni nyingi, na ulipovunja mojawapo, uliingia kwenye mashaka. Ingawa Mungu anakusudia tuzingatie sheria zake, anaelewa jinsi tulivyo na yuko tayari kumwonyesha yeyote fadhila yeyote atakayeomba na kupokea.

Tukijifunza kupokea fadhila, basi nasi pia tutaweza kuwapa wengine—na fadhila ni kitu ambacho watu wengi hutaka sana.


Sala ya Shukrani

Asante, Baba, kwa vile unavyonipa fadhila kila siku. Ninatamani kukupendeza katika kila kitu ninachofanya, lakini ninakushukuru kuwa ninapopungukiwa, hukosi kunibariki kwa kipaji chako cha bure cha upendo na fadhila.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon