Sifa Kuu za Mungu

Sifa Kuu za Mungu

Wataua na waushangilie utukufu, waimbe kwa sauti kuu vitandani mwao. Sifa kuu za Mungu na ziwe vinywani mwao, na upanga mkali kuwili mikononi mwao. —ZABURI 149:5– 6

Tunafaa kuwa na tabia ya kushukuru na kusifu Mungu punde tunapoamka kila asubuhi. Kama bado tumelala vitandani, acha tumpe Mungu shukrani na kujaza maandiko katika mawazo yetu.

Sifa humshinda shetani haraka kuliko mpango mwingine wowote wa vita. Sifa ni vazi lisiloonekana ambalo huwa tunavaa na kutukinga kutokana na kushindwa pamoja na uhasi katika fikra zetu. Lakini lazima iwe ya kweli, sifa ya kutoka moyoni, sio tu midomoni au mbinu inayojaribiwa ili kuona kama itafanya kazi. Tunamsifu Mungu kwa ahadi zilizo katika Neno lake na kwa wema wake.

Sifa ni mahali pa vita! Tunapomsifu Mungu kwa jinsi alivyo na kwa sifa zake, kwa uwezo na nguvu zake, tunasonga karibu naye na adui anashindwa.

Tunaweza kuwa tu na wingi wa shukrani! Kushukuru Mungu mchana kutwa na kukumbuka mambo mengi ambayo amekutendea.


Mungu huwa hashindwi vitani. Ana mpango maalum wa vita, na tukimfuata, tutakuwa tukishinda wakati wote.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon