Sikiza na Roho Yako

Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima (YOHANA 6:63)

Wakati mwingine nafsi zetu, hiari au hisia huingilia uwezo wetu wa kusikia sauti ya Mungu. Tunapojaribu kumsikia na kumtii Mungu, fikra hasi zinaweza kutushambulia kufikia kiwango cha kuhisi kusalimu amri. Lakini tukituliza akili zetu na kuona kilicho mioyoni mwetu, Mungu atatupatia hakikisho la kile anasema. Tutahisi jibu lake likiinuka na amani pamoja na uhakikisho kutoka ndani kabisa ya mioyo yetu ambapo Roho Mtakatifu huishi.

Wakati mmoja nilikuwa nimemaliza mkutano, mkutano ambao nilikuwa nimeufanyia bidii sana kuhakikisha kwamba unasaidia watu waliouhudhuria. Ingawa kila mtu alionekana kuufurahia, niliendelea kusikia katika mawazo yangu, “Hakuna aliyebarikiwa na wengi walijuta kuja.”

Nilihisi kama mshinde dhaifu, ambayo nilijua hayakuwa mapenzi ya Mungu kwangu mimi, kwa hivyo nikakimya na kutulia na kusikiliza kile ambacho Roho Mtakatifu angeniambia. Punde tu nikasikia ile sauti ndogo yenye kimya, inayojua undani wa ndani, ikisema, “Iwapo watu hawakutaka kuwa hapa, hawangekuja. Iwapo hawangekuwa wanafurahia, wengi wangeondoka. Nilikupa ujumbe, na huwa simpi yeyote ujumbe mbaya kuhubiri, kwa hivyo usimruhusu shetani kuiba furaha ya kazi yako.” Nisingesikiza, ningeendelea kutaabika, lakini neno la Mungu likaniletea uhai.

Tunasikia kutoka kwa Mungu kupitia kwa roho zetu, sio kwa mawazo yetu. Kumbuka hilo, na uchukue muda kila wakati kutulia na kumwuliza Mungu anachosema kwa kweli.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Neno la Mungu huleta uhai wakati wote.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon