Tunapomhitaji Zaidi

Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, wala usizitegemee akili zako mwenyewe, katika njia zako zote mkiri yeye, naye atanyosha mapito yako. —MITHALI 3:5– 6

Mara nyingi huwa tunasema kwamba tunamwamini Mungu, lakini ndani bado tuna hofu iliyokita mizizi kwamba kwa kweli hatatusaidia tutakapomhitaji sana. Kwa hivyo, kwa kutokujua tuna chukulia kwamba tukiendelea kufikiria kuhusu shida hiyo na kuwa na wasiwasi, basi tunaweza kuishughulikia wenyewe—iwapo tu Mungu hatatusaidia na kufanya kitu kulingana na ratiba yetu.

Shida ya wazo kama hili ni kwamba linatuleta karibu na shida zetu, na sio karibu na Mungu. Lakini tukichagua kuamini kuwa Mungu yuko usukani na kwamba atashughulikia shida yoyote tuliyo nayo, tunamkaribia Mungu na shida zetu zinakosa kututia wasiwasi hata hivyo.

Kuamini Mungu kutakuzuia kuwaza kuhusu mambo ambayo hauna majibu yake bado. Ukikabiliwa na hali ngumu, usisikilize ile sauti sumbufu ndani yako, ikiuliza, Utafanya nini? Utafanya nini? Jikumbushe tu kwamba, nitamwamini Mungu, na atanionyesha la kufanya… iwapo nahitaji kufanya chochote.


Kuwa na amani, tulia na Mungu atakupigania.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon