Ubatizo wa Moto

Kweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi wala sistahili hata kuvichukua viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto (MATHAYO 3:11)

Kama waaminiyo, tumeitwa kufanya mengi zaidi ya kwenda kanisani Jumapili asubuhi, kufanya zaidi ya kufuata kaida zilizoamriwa, na bila shaka kufanya mengi zaidi kuliko kunyunyiziwa maji vichwani mwetu au kutumbukizwa katika vidimbwi vya ubatizo. Hayo yote ni muhimu sana na hayafai kupuuzwa, lakini lazima yafuatiwe na hiari ya tajriba ya “ubatizo wa moto.”

Huku akimjibu mama yake Yakobo na Yohana, ambaye alikuwa ameuliza iwapo wanawe wangeketi mmoja, mkono wake wa kuume na mwingine mkono wake wa kushoto atakapokuja katika Ufalme wake (soma Mathayo 20:20-21), Yesu alijibu kwamba hawakujua walichokuwa wakiomba. Alisema, “Hamjui mnaloliomba. Je! Mwaweza mwaweza kunywea kikombe nitakachonywea mimi?” (Mathayo 20:22).

Ni ubatizo gani ambao Yesu alikuwa anazungumzia? Alikuwa tayari ashabatizwa katika Mto Yorodani na kupokea ubatizo wa Roho Mtakatifu wakati huo huo (soma Marko 1:9- 11). Ni ubatizo gani mwingine uliopo?

Yesu alikuwa anasema kuhusu ubatizo wa moto. Moto ni ajenti ya kutakasa, kitu ambacho husababisha kutotulia huku kikifanya kazi. Yesu hakuwa na dhambi na, kwa hivyo, hakuhitaji kutakaswa; lakini tunahitaji. Yesu ndiye hutubatiza na Roho Mtakatifu na moto.

Kuwa na ujasiri wa kumwomba Yesu kukubatiza na moto wake. Mwombe afanye kazi ya kusafisha na kutakasa ndani yako ili uwe chombo kinachostahili kutumiwa naye. Huenda ikawa vigumu kuupitia, lakini utaleta tuzo la kuridhisha.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Unapopitia kwa moto, Mungu atakuwa nawe. Hatakuacha wala kukusahau.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon