Tazama, jinsi ilivyo vema, na kupendeza, ndugu wakae pamoja kwa umoja… kama umande wa Hermoni usshukao milimani pa Sayuni. Maana ndiko Bwana alikoamuru baraka, naam, hata milele (ZABURI 133:1, 3)
Unapokuwa umeomba kuhusu kitu na huonekani kusikia kutoka kwa Mungu, huenda ukahitaji kutafuta mtu wa kuomba kwa kukubaliana naye. Aina hiyo ya umoja ina nguvu za kiroho, na kulingana na andiko la leo, ni vizuri na huamrisha baraka ya Bwana.
Watu wawili au zaidi wanapoingia katika makubaliano, Yesu anaahidi kuwa nao, na uwepo wake kutumia nguvu zaidi kuliko tunayoweza kufikiria katika maisha na hali zake. Anasema katika Mathayo 18:19-20: “Tena nawaambia ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lolote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni. Popote wawili au watatu wanapokusanyika (kuja pamoja kama wafuasi wangu) kwa jina langu, hapo nitakuwa katikati yao.” Mungu yuko na kila moja wetu pia, lakini nguvu zetu huzidi tunapokuja pamoja katika umoja na makubaliano. Biblia inasema, mmoja angefukuzaje watu elfu, wawili wangekimbizaje elfu kumi (Kumbukumbu la Torati 32:30). Ninapenda aina hiyo ya hisabati!
Kwa sababu baraka ya Mungu hutulia juu ya amani na uwepo wake uko juu ya wale wanaokubaliana katika jina lake, adui hufanya kazi kwa bidii ili kugawanya watu, kuleta ugomvi katika mahusiano, na kukosanisha watu. Tunahitaji kuelewa nguvu za umoja na makubaliano, na tunahitaji kufanya mazoezi ya nguvu hizo kwa kuzungumza na Mungu na kutafuta sauti yake na wengine.
NENO LA MUNGU KWAKO LEO:
Usiache kuomba na wengine.