Umuhimu wa Fikra Sahihi

Umuhimu wa Fikra Sahihi

Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo. MITHALI 23:7

Nafsi ndio kiongozi au kitangulizi cha matendo yote. Hatua tunazochukua kila siku ni matokeo ya moja kwa moja ya fikra tunazojiruhusu kufikiri.

Ikiwa tuna nafsi hasi, tutakuwa na maisha hasi. Kwa upande ule mwingine, tukizigeuza upya nia zetu kulingana na neno la Mungu, tutashuhudia “mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu” kwa maisha yetu (Warumi 12:2).

Matatizo ya watu wengi yana misingi yake katika ruwaza za fikra zisizo sahihi. Kwa kweli fikra hasi zinaweza kuwafanya wajiletee matatizo wanayoyapitia katika maisha yao; hata hivyo tunashukuru kuwa si lazima tuishi tukiwa wafungwa wa mawazo hayo. Tunaweza kuchagua kuelekeza mawazo yetu yalingane na Neno la Mungu.

Nafsi ni uwanja wa vita. Amua kupinga fikra hasi haribifu na fikra zako ziwe za kiungu badala yake. Kadri unavyobadilisha nafsi yako kwa ajili ya mema, ndivyo maisha yako yatabadilika kwa wema.


Sala za Shukrani

Baba, ninashukuru kwamba silazimiki kuishi kama mfungwa wa fikra zangu. Kwa usaidizi wako, ninaweza kubadilisha hizo fikra hasi zinazoathiri maisha yangu. Ninaweza kushinda vita vya nafsi yangu kwa kutumia wakati kusoma Neno lako, kutafakari juu ya ahadi zako, na kuamua kuwaza fikra zinazomtukuza Mungu juu ya maisha yangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon