Unapojihisi Kukosa Usalama

Unapojihisi Kukosa Usalama

Kristo akae mioyoni mwenu kwa imani mkiwa na shina na msingi katika upendo. —WAEFESO 3:17

Watu wengi wana hisia za kutokuwa salama kujihusu kwa sababu hawawezi kujikubali tu vile walivyo. Je, umechoka kushinikizwa, na kujifanya kuwa mtu usiye? Kwani hungependa uhuru wa kukubaliwa vile tu ulivyo? Bila mshinikizo wa kuwa mtu ambaye hujui kuwa kama yeye?

Kwa usaidizi wa Mungu, tunaweza kujifunza thamani yetu haiko katika kile tunafanya lakini kile tulicho ndani yake. Anataka tuje kwake jinsi tulivyo na kuamini atatusaidia kuwa kila kitu anachotaka tuwe.

Mpango wa shetani ni kutudanganya kufikiria kwamba thamani yetu iko katika matendo yetu, halafu atufanye kuzingatia makosa na udhaifu wetu. Shetani anataka tujione duni ili tuondoke kwa Mungu, tuwe na dhiki na tushindwe kupokea baraka zake, kwa sababu tunafikiri hatustahili kuzipata.

Ni muhimu kuanza kuwa na fikra kwamba tuna thamani, na kuwa salama ndani ya Kristo. Fanya uamuzi wa kujikubali kwa sababu hilo ndilo Yesu amefanya tayari. Hatawahi kukataa mtu yeyote anayekuja kwake. Unapendwa na kuthaminiwa sana!


Mungu anajua makosa yako lakini anakupenda vivyohivyo. Hakuna kitakachobadilisha upendo wake kwako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon