Unaweza kuwa Mwaminifu kwa Mungu

Unaweza kuwa Mwaminifu kwa Mungu

Ikawa alipokuwa mahali fulani akiomba, alipokwisha, mmoja katika wanafunzi wake alimwambia, Bwana tufundishe sisi kusali, kama vile Yohana alivyowafundisha wanafunzi wake. —LUKA 11:1

Maombi yenye mafanikio hayakuzwi kwa muda wa usiku mmoja wala hayawezi kuigwa kutoka kwa mtu mwingine. Mungu ana mpango binafsi wa kila mmoja wetu. Hatuwezi wakati wote kuwa tukifanya kile mtu mwingine anafanya na kutarajia kwamba tutafanikiwa. Maisha yetu ya maombi ni ya kuendelezwa—huendelea tunapozidi kuendelea.

Mara nyingi maombi yetu huwa sio dhahiri, kumaanisha huwa hayaelezwi kwa uwazi. Tunapoomba tunaweza kuwa dhahiri na waaminifu kwa Bwana. Biblia inafunza kwamba tunaweza kuomba kwa ujasiri, kwa matarajio na kwa kulenga. Baba yako wa mbinguni anakupenda, kwa hivyo unaweza kuja kwake bila hofu, kwa hakika na ujasiri kwa kiti cha neema (Waebrania 4:16).

Ukihitaji usaidizi katika maisha yako ya maombi, kuwa mwaminifu kwa Mungu, mwambie mahitaji yako. Atakusaidia ukimwomba afanye hivyo. Kama wanafunzi, omba tu “Bwana, nifundishe kuomba.”


Ufunguo muhimu wa maombi ni uhakika zaidi katika jina la Yesu na uhakika mchache ndani yetu au mtu mwingine yeyote kutusuluhishia shida zetu. Kuna nguvu katika jina la Yesu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon