Upendo dhidi ya Hasira

Upendo dhidi ya Hasira

Wapenzi na mpendane kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu na kila apendaye amezaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu. 1 YOHANA 4:7

Hasira ni hisia ya nguvu, lakini upendo una nguvu zaidi. Na upendo ndio kielelezo ambacho Mungu amedhihirishia kila mmoja.

  • Katika hasira, tunaweza kukosoa, lakini katika upendo, tunahimiza.
  • Katika hasira huenda tukageuka na kwenda, lakini katika upendo, tunafikia mtu.
  • Katika hasira, tunaweza kuwa wachoyo, lakini katika upendo, tunakuwa wakarimu.
  • Katika hasira, tuna jicho la hasira, lakini katika upendo, tunatabasamu
  • Katika hasira, tunalaumu, lakini katika upendo, tunasamehe.

Mojawapo ya njia nzuri kabisa ya kuonyesha shukrani zako kwa Mungu ni kuwaonyesha wengine upendo huo. Usiwe tu mpokeaji wa upendo wa Mungu; kuwa mpaji wa upendo huo kwa wote unaotangamana nao.


Sala ya Shukrani

Asante, Baba, kwa dhihirisho la upendo ulilonionyesha ili nifuate. Ninashukuru kwamba unanipenda, na kwa usaidizi wako nitawaonyesha wengine upendo huo huo.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon