Upendo Huvumilia

Upendo Huvumilia

Upendo huvumilia kwa muda mrefu… —WAKORINTHO 13:4

Ulimwengu leo umejaa watu wasio na subira. Huonekana kwamba kila mtu yuko mbioni. Viwango vya msongo wa mawazo viko juu sana, na mshinikizo tunaoishi chini yake huchochea kukosa uvumilivu. Wakristo hukabiliana na mishinikizo hiyo kama watu wengine, na mara nyingi huwa tunakosa uvumilivu kama tu ulimwengu, lakini hatufai kuwa hivyo.

Biblia inatufundisha kwamba upendo huvumilia. Kadri tunavyojifunza kupokea upendo wa Mungu, kumpenda pia, na kuwapenda walio karibu nasi, ndivyo tunavyokuwa wenye uvumilivu zaidi. Huu uvumilivu hutusaidia kuishi kwa amani. Na kukosa kuwa mbioni. Tunachukua muda kumngoja Mungu na kuwa na ushirika naye. Kutokana na upendo wake, Mungu ana subira nasi na tunaweza kuwa vivyo hivyo na watu wengine.

Maisha yako yakiwa na alama ya upendo, hutakuwa tu mwenye uvumilivu kwa watu wengine, utakuwa mwenye uvumilivu kwako mwenyewe. Ukifanya makosa, badala ya kujikasirikia kuhusu makosa hayo, utatubu na kukaa kwa amani. Utaelewa kwamba Mungu anafanya kazi kurekebisha vitu hivyo katika maisha yako, na utamtumainia kwa uvumilivu kufanya kazi yake.

Uvumilivu ni adili zuri linaloweza kukuzwa katika masiha yako, lakini ufunguo ni kumkaribia Mungu kupitia kwa kuamini kila siku na siku zote. Kadri unavyomkaribia Bwana, ndivyo inavyokuwa rahisi kwako kuachilia dhiki za ulimwengu. Utapata hisia mpya za utulivu na hakikisho lenye amani kwa sababu Mungu ni kitovu cha maisha yako.


Ukijifunza kukabiliana na aina zote za majaribu kwa uvumilivu, utajipata ukiishi kiwango cha maisha ambacho hakivumiliwi tu bali pia kinafurahiwa kikamilifu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon