Upendo usio na Masharti

Upendo usio na Masharti

Na amri hii tumepewa na yeye, ya kwamba yeye ampendaye Mungu, ampende na ndugu yake. —1 YOHANA 4:21

Kulingana na Neno la Mungu, alitupenda kabla ya kuumba ulimwengu, kabla tumpende au kumwamini au kuwahi kufanya kitu chochote kizuri au kibaya. Si hilo linashangaza? Upendo wa Mungu ulikuwa, umekuwa, na wakati wote utakuwa usio na mwisho wala masharti.

Kwa sababu Mungu hatuhitaji kuchuma upendo wake, tunaweza kufuata mfano wake, bila kuhitaji wengine wachume upendo wetu. Upendo sio kitu tunachofanya na kutofanya. Hatufai kuwa nao na kutokuwa nao kutegemea tunayetaka kumpa na vile wanavyotutendea. Kama waaminio ndani ya Yesu, upendo tunaoweza kuonyesha ulimwengu ni upendo wa Mungu usio na masharti unaotiririka kutoka kwetu hadi kwao. Hatuwezi kuelewa aina hii ya upendo wa Mungu kwa mawazo yetu. Unapita maarifa yote. Ni ufunuo ambao Mungu huwapa wanawe. Ni kitu tunachohisi tunapomkaribia Bwana, na ni kitu ambacho huwa tuko tayari kueleza watu walio karibu nasi kukihusu.

Upendo usio na masharti huamini mema kuhusu watu. Huwa unaona kile wanachoweza kuwa iwapo mtu atawapenda. Hivyo ndivyo Mungu alitutendea. Aliamini mema na kuona kwamba upendo wake usio na masharti ungetubadilisha tuwe mfano wa Mwanawe.


Ukipokea upendo wa Mungu bure, utaweza kutoa bure huohuo upendo.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon