Upendo wenye Wivu

Au mwadhani ya kwamba maandiko yasema bure? Huyo Roho akaaye ndani yetu hututamani kiasi cha kuona wivu? (YAKOBO 4:5)

Andiko la leo linatoa muhtasari wa ukweli kwamba Roho Mtakatifu anataka kukaribishwa katika maisha yetu. Kwa kweli anatamani kuwa na ushirika nasi.

Kulingana na Yakobo 4:4, ambayo inatangulia andiko la leo, tunaposhughulika na vitu vya ulimwengu kuliko vile tunavyoshughulika na Mungu, anatuona kama wake wasioaminika, wakiwa katika mapenzi haramu na ulimwengu na kuvunja kiapo cha ndoa naye. Ili kutufanya kuwa waaminifu kwake, analazimika kuondoa vitu katika maisha yetu anapoona kwamba vinatuzuia kuwa naye.

Tukiruhusu kazi kuja kati yetu na Mungu, huenda tukaipoteza. Pesa zikitutenganisha naye, huenda tukagundua kwamba itakuwa bora kwetu kuwa na pesa chache na vitu kuliko kutenganishwa na Mungu. Mafanikio yakitatiza uhusiano kati yetu na Baba yetu wa mbinguni, huenda tukashushwa badala ya kupandishwa. Iwapo marafiki zetu watachukua nafasi ya kwanza dhidi ya Mungu katika maisha yetu, huenda tukawapoteza baadhi yao.

Wingi wa watu hukosa kugundua kwamba, huwa hawapokei vitu wanavyotaka kwa sababu kwa kweli hawamtangulizi Mungu. Mungu huona wivu juu yako: Anataka nafasi ya kwanza katika maisha yako. Hakuna kingine kitakachokuwa kibadala chake.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO: Mwambie Mungu aondoe chochote katika maisha yako kinachochukua nafasi yake.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon