Usijipeane kwa huruma

Usijipeane kwa huruma

Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho Yeremia 29:11

 Kujionea huruma ni hisia yenye uharibifu na hasi. Inatufichia baraka zetu na uwezekano mbele yetu na huiba tumaini letu lote la leo na kesho. Watu ambao hujihurumia mara nyingi hufikiri, Kwa nini nijaribu kufanya chochote? Mimi nitashindwa tu.

Kujionea huruma ni sawa na ibada ya sanamu kwa sababu ni mtazamo wa kibinafsi uliofanywa kupita kiasi. Tunapojiruhusu kubaki katika huruma, tunakataa upendo wa Mungu na uwezo wake wa kubadilisha mambo.

Ninakuhimiza usipoteze siku moja zaidi ya maisha yako kwa kujihurumia. Unapopoteza matumaini na kuanza kujisikia huruma, simama na useme: “Ninakataa kujisikia huruma. Huenda nikawa katika msimu mgumu wa maisha hivi sasa, lakini siwezi kuacha kutumaini mambo mazuri! ”

Mungu ana mawazo na mipango mema kwako, kukupa tumaini kwa siku zijazo zako. Ikiwa utashikilia tumaini lako kwa kuweka lengo lako na imani katika Yesu, mambo ya ajabu yatatokea katika maisha yako!

OMBI LA KUANZA SIKU

Mungu, mimi nakataa kujionea huruma. Wakati hali ni ngumu, nitakumbuka kwamba wewe ni mkuu zaidi kuliko matatizo yangu na una hatima nzuri iliyopangwa kwa ajili yangu. Nataka mipango yako ifanyike katika maisha yangu, na ninaweka imani yangu kwako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon