Usiwe na hofu

Usiwe na hofu

Bwana akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha;  Mwanzo 12:1

Biblia inasema juu ya mtu mmoja aitwaye Abramu aliyemwamini Mungu licha ya hofu yake mwenyewe.

Je! Ungehisije kama Mungu alikuambia uondoke nyumbani kwako, familia yako na kila kitu ambacho ni kizuri na cha starehe na uende  mahali pasipo julikana? Utajawa na hofu? Hiyo ndivyo Mungu alivyomwambia Abramu kufanya-na aliogopa. Lakini maneno ya Mungu kwake yalikuwa “Usiogope.”

Mara nyingi tunadhani tunapaswa kusubiri kufanya kitu wakati hofu imeisha, lakini ikiwa tutafanya hivyo, tutafikia kidogo sana kwa Mungu, kwa wengine, au hata kwetu wenyewe. Abramu alipaswa kuingia katika imani na kumtii Mungu, licha ya hofu yake.

Ikiwa Abramu angeiinamia hofu, kamwe hangekamilisha hatima yake kuwa Mungu yote alimwumba awe-baba wa mataifa mengi.

Kukubaliana na hofu kunabadili mpango bora zaidi wa Mungu kwa maisha yako, hivyo fanya kile anachotaka ufanye … hata kama unafanya hivyo kwa hofu! Kama Abramu, utapata kwamba tuzo yake ni nzuri.

OMBI LA KUANZA SIKU

Mungu, Wewe ulikuwa mwaminifu kwa Abramu wakati alipokusikiliza licha ya hofu, kwa hiyo mimi pia nitaamua kupinga hofu na kufanya chochote unachoniambia nifanye.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon