Utafanya Uteuzi Gani?

Utafanya Uteuzi Gani?

Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima ili uwe hai, wewe na uzao wako. KUMBUKUMBU LA TORATI 30:19

Yesu anataka tuwe na furaha katika mioyo yetu. Ni muhimu kwa afya yetu ya kimwili, kiakili, kihisia na kiroho. Hii ndiyo kwa sababu Mithali 17:22 inasema, “Moyo uliochangamka ni dawa nzuri; bali roho iliyopondeka huikausha mifupa.” Ni mapenzi ya Mungu kwetu kufurahia maisha.

Ni wakati wa kuamua kuingia katika maisha timilifu yaliyofurika ambayo Mungu anahiari juu yetu. Tunaweza kuwa wenye shukrani kwamba Mungu huturuhusu kuchagua aina ya maisha ambayo tunataka kuishi. Furaha na kuburudika, vipo kama tu ilivyo dhiki na huzuni. Haki na amani ipo, lakini pia shutuma na fujo. Kuna baraka na laana pia, na ndiyo kwa sababu Kumbukumbu la Torati 30 inatuambia tuchague mojawapo.

Fanya uteuzi mzuri leo. Chagua Yesu. Chagua furaha. Chagua amani. Chagua uzima!


Sala ya Shukrani

Baba, ninakushukuru kwamba ninaweza kuchagua kiwango cha maisha ninachotaka ili kukuishia. Nisaidie kufanya uamuzi wa hekima leo. Nisaidie kuchagua amani na furaha. Ninajua kwamba utanipa amani na kuniongoza katika kila hatua njiani. Wasiwasi hauna maana na ninaamua kutoharibu muda kwa kuwa nao!

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon