Wakati kuombea wengine ni ngumu

Wakati kuombea wengine ni ngumu

Wabarikieni wale ambao wawalaani ninyi, waombeeni wale ambao wawaonea ninyi. Luka 6:28

Unajibuje wakati mtu anaumiza hisia zako? Je! Unairuhusu iibe furaha yako? Au je, hisia zako zinalipuka?

Luka 6:28 inatuambia kile tunachopaswa kufanya wakati watu wanatuumiza: Lazima tuwaombee na kuwabariki.

Sio jambo la asili kuwaombea furaha wale wanaokulaani. Lakini hekima ya Mungu ni ya juu kuliko yetu, hivyo kwamba ingawa hatuhisi “sawa,” ni jambo la haki ya kufanya. Nami nina nia ya kufanya hivyo kwa utiifu na kusema, “Bwana, sijisikii  kubariki watu ambao wananiumiza, lakini nataka kuomba kwa imani kuwa Wewe utafanya hivyo, kwa sababu unaniambia kuwabariki kwa uwepo wako. ”

Uchaguzi wa kuwaombea ni moja ya mambo magumu sana ambayo Mungu anatutaka tufanye, hasa ikiwa tunaamini kwamba yeyote anayetuumiza ni mkosaji na hastahili kusamehewa.

Lakini Mungu anatuamuru tuwasamehe. Na tunapochagua kufuata njia ya msamaha, tutapata amani na furaha ambayo huja kwa kulitii Neno la Mungu. Unapomtii Mungu, anaweza kukusaidia kushinda maumivu ya makosa na kufurahia maisha zaidi.

OMBI LA KUANZA SIKU

Mungu, ni vigumu, lakini ninawaombea wale walioniumiza na kukuomba Uwabariki. Nisaidie kuachilia uchungu na kuwasamehe.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon