Wakati Wote Kuna Muda wa Maombi

Wakati Wote Kuna Muda wa Maombi

Wakapaza sauti wakisema, Ee Yesu, Bwana mkubwa, uturehemu! LUKA 17:13

Hata ikiwa wewe ni mama, mwalimu, meneja, fundi wa mitambo au daktari mpasuaji ubongo, bila shaka una shughuli nyingi! Utakuwa na mahitaji ya kazi yako kutekeleza pamoja na wajibu wako kwa familia na jamaa zako. Haijalishi shughuli utakazokuwa nazo, jipe moyo: Mungu husikia maombi yote—hata mafupi—na hicho ni kitu cha kushukuru!

Maombi ni kitu unachoweza kufanya siku yote hata kama una orodha ndefu ya mambo ya kufanya. Kwa mfano, iwapo wewe ni mama uliyechoka ambaye hushinda nyumbani na kubadilisha nepi siku yote, basi tenga tu dakika moja kutulia na useme, “Oo Yesu, ninakupenda. Nitie nguvu sasa hivi. Mungu, ninahitaji nguvu. Nimechoka.”

Ni sawa kutumia njia rahisi sana kuongea na Mungu. Kwa kutumia siku nzima tukiomba kwa njia rahisi inayoleta maana, tunamwalika Mungu katika kila eneo la maisha yetu, na hivyo ndivyo anavyotaka.


Sala ya Shukrani

Ninakushukuru leo, Baba, kwamba si lazima maombi yawe marefu na yenye utata. Unasikia pia maombi yangu mafupi yanayotoka moyoni. Nina shukrani kwamba ninaweza kuendeleza mazungumzo nawe kwa siku nzima, na kwamba unasikia na kunijibu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon