Watu ni wa Mungu

…Usiogope, maana nimekukomboa; nimekuita kwa jina lako wewe u wangu (ISAYA 43:1)

Una kitu ambacho ni cha thamani sana kwako, unachopenda sana na kustahi? Ukiona mtu akikizungusha kila mahali kiholela au kukihatarisha na uharibifu, si utahuzunika?

Mungu huhisi hivyo hivyo kuhusu vitu vyake jinsi tunavyohisi kuhusu vyetu. Watu ni mali ya Mungu. Ni viumbe wake na Roho wake huhuzunika anapoona wakiteswa.

Sio kila mtu ana wito unaofanana na wa mwingine katika maisha, lakini kila mtu aliyezaliwa upya ni mrithi wa Mungu na mrithi pamoja na Kristo. Kila mtu ana haki ya amani, haki, na furaha; mahitaji yao kutimizwa, kutumiwa na Mungu, na kuona upako wake ukitiririka kupitia kwao.

Kila mtu ana nafasi sawa ya kuona matunda katika huduma yake, lakini hiari yao ya kuwapenda wengine huamua kiasi cha matunda watakayoyaona. Roho Mtakatifu alizungumza nami katika miaka iliyopita: “Mojawapo ya sababu kuu zinazofanya watu kutotembea katika upendo ni kwamba unahitaji bidii. Kila mara wanapotembea katika upendo watagharamika.”

Upendo hutuhitaji kuzuia kusema vitu vingine ambavyo tungesema. Upendo unadai tusifanye vitu vingine ambavyo tungependa kufanya na kwamba tupeane vitu vingine ambayvo tusingependa kupeana. Upendo hutuhitaji kuwa na subira na watu.

Mahusiano si rahisi kila wakati, lakini ni muhimu kwa Mungu kila wakati kwa sababu anathamini watu. Tunahitaji kujitolea na kufanya bidii inayohitajika ili kupenda watu kwa kuwa Mungu anataka tuwapende ili tusimhuzunishe.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Mungu huona watu kama hazina yake, kwa hivyo jihadhari na vile unavyowatendea.  

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon