Wepesi wa Furaha na Amani

Wepesi wa Furaha na Amani

Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu —WARUMI 14:17

Miaka mingi iliyopita, nilikuwa na wazo hili: Maisha hayafai kuwa magumu hivi. Kuna kitu kilichojificha ndani yangu, huku kikinyonya furaha yangu. Ikaanza kuniwia wazi kwamba nilikuwa nikishuku badala ya kuamini. Nilikuwa nikishuku mwito wa Mungu juu ya maisha yangu, huku nikishangaa iwapo angekutana na mahitaji yetu, nikitia doa maamuzi na matendo yetu.

Nilikuwa na fikra mbaya badala ya fikra nzuri. Nilikuwa ninashuku badala ya kuamini.

Shaka hufanya mambo yote yawe magumu. Inapenya ndani kupitia kwa mlango wa moyo wako, huku ikijaza mawazo yako na fikra za kiakili zinazosababisha fikra hasi. Inazungukia kwenye hali na mambo hayo hayo ya maisha yako, ikijaribu kuyatafutia suluhu.

Neno la Mungu halituagizi kutafuta suluhu zetu wenyewe. Hata hivyo, tunaagizwa kuamini Mungu kwa mioyo na nafsi zetu zote (Mithali 3:5). Tukifuata mwongozo rahisi ambao Bwana ametupatia, bila kukosea utatuleta karibu naye, na kutusababisha kuishi kwa furaha na amani.

Shaka inapobisha mlangoni pako, jibu kwa moyo wa kuamini, na utahakikishiwa ushindi wakati wote.


Furaha huwa haiachiliwi kupitia kwa kutokuamini lakini huwepo palipo na kuamini wakati wote.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon