Zaa Matunda Mema

Hivyo hutukuzwa Baba yangu, kwa vile mzaavyo sana, nanyi mtakuwa wanafunzi wangu (YOHANA 15:8)

Katika andiko la leo, Yesu alisema kwamba Mungu hutukuzwa tunapozaa matunda. Alizungumzia pia kuhusu matunda katika Mathayo 12:33 aliposema kwamba miti hujulikana kwa matunda inayozaa, na katika Mathayo 7:15-16 alitumia kanuni hii hii kwa watu. Haya maandiko yanatuonyesha kwamba kama waaminiyo, tunahitaji kujali kuhusu aina ya matunda tunayozaa. Tunataka tuzae matunda mema ya Roho Mtakatifu (soma Wagalatia 5:22-23), lakini tutafanyaje hivyo?

Tunajua kwamba Mungu ni moto ulao, na kwamba Yesu alitumwa kutubatiza na Roho Mtakatifu pamoja na moto. Hadi turuhusu moto wa Mungu kuwaka katika maisha yetu, hatutawahi kudhihirisha matunda ya Roho Mtakatifu.

Kuzaa matunda mema huonekana kusisimua hadi tunapotambua kwamba kuzaa matunda kunahitaji kupunguzwa. Yesu alisema: “Kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na kila tawi lizaalo hulisafisha ili lizidi kuzaa” (Yohana 15:2). Jinsi tu moto unavyoeleza kazi ambayo Roho Mtakatifu hufanya katika maisha yetu, basi moto vilevile. Moto ni muhimu kwa kusafisha na kifo cha mwili; kupunguzwa ni muhimu kwa ajili ya ukuaji. Lazima vitu vilivyokufa na vitu vinavyoenda upande mbaya viondolewe ili tukue kama “miti ya haki” na kumzalia Mungu matunda yenye utajiri (Isaya 61:3).

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Mungu akiondoa kitu katika maisha yako, hufanya hivyo ili kutengeneza nafasi ya kitu bora zaidi.  

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon