Kuwaza Fikra Nzuri

Kuwaza Fikra Nzuri

. . . Mambo yoyote yaliyo ya kweli, yoyote yaliyo ya staha, yoyote yaliyo ya haki, yoyote yaliyo safi, yoyote yenye kupendeza, yoyote yenye sifa njema, ukiwapo wema wowote, ikiwapo sifa nzuri yoyote, yatafakarini hayo. —WAFILIPI 4:8

Ukitaka kuboresha maisha yako, mojawapo ya vitu vya kwanza unavyoweza kufanya ni kuboresha mawazo yako. Kuna nguvu kuu zinazokuja tunapochagua kuwa watu wanaowaza mawazo mema. Mungu huwaza mema, na ili tumkaribie, ni muhimu kukubaliana naye (Amosi 3:3) na kuwaza mema.

Kuwa nia njema na mawazo haimaanishi kwamba hukabiliani na ukweli au unapuuza ukweli wa matatizo. Inamaanisha tu kwamba unakubaliana na Neno la Mungu na kukaa ndani ya ahadi za Mungu badala ya mawazo mabaya, na vitu vinavyotamausha vya ulimwengu.

Tambua kwamba katika maisha yake yote, Yesu alivumilia mambo magumu sana, yakiwemo mashambulizi ya kibinafsi ilhali alikuwa na mawazo mema. Alikuwa akitoa neno la kuinua wakati wote, na neno la kuhimiza. Alitoa tumaini kwa wale aliyokuja karibu nao wakati wote. Tunaweza kufuata mfano huo leo. Tunapochagua kuwa na mtazamo chanya, kudumisha matarajio mema, na kujihusisha katika mazungumzo mema, tunafuata mfano ambao Yesu alitupatia, na tunazidi kumkaribia Baba yetu wa mbinguni.


Maisha yako yatafuata mwelekeo wa mawazo yako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon